Jumamosi 12 Aprili 2025 - 17:57
Siku mwanafunzi wa dini au wa sekular anaposema "Nimehitimu", hiyo ndio siku ya kuangamia kwake

Ayatollah Jawadi Amoli alisema: "Kamwe katika elimu na maarifa usiangalie watu walio chini yako, bali angalia wale walio juu yako."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Jawadi Amoli katika makala yake aliandika kuhusu Hadithi inayo sema “لا شرف كبعد الهمة” na kusema:

"Mwanadamu muda wa kuwa yupo hai, lazima aendelee kujifunza, kufundisha, na kushughulika na vitabu. Siku ambayo mwanafunzi wa dini au wa sekular atasema "nimehitimu" na kuweka pembeni vitabu, ataangamia. Muda wa kuwa unapumua, lazima uendelee kuelewa kwamba elimu haina mipaka, kamwe usiangalie wale waliopo chini yako katika elimu na maarifa, bali angalia wale waliopo juu yako."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha